Thursday, 6 January 2011

Rostam Aziz aikana Richmond

KAULI aliyoitoa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa imemuibua Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Rostam alikanusha maelezo ya Dk. Slaa aliyemhusisha na tuhuma za kuhusika kwake kuileta nchini kampuni ya Richmond nchini kutoka nchini Marekani.
Dk. Slaa ambaye kauli yake ilichapwa katika gazeti hili juzi alisema Richmond ililetwa nchini baada ya Rais Jakaya Kikwete na Rostam kwenda Marekani kwa malengo hayo kwa safari mbili tofauti.
Akijibu shutuma hizo, Rostam alikanusha kwenda nchini Marekani wakati wa mchakato wa kuileta Richmond nchini na akasema kwa mara ya mwisho alikuwa nchini humo Desemba mwaka 2008.
Kwa habari zaidi soma : http://www.tzuk.com/index.php?option=com_content&task=view&id=4567&Itemid=105

No comments:

Post a Comment