Wednesday, 10 November 2010

Kwa nini CCM kimeporoka?


PAMOJA na maandalizi kabambe ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti ya kampeni hadi kufikia Sh50bilioni, kimepata matokeo mabaya zaidi tangu kuanza kwa uchaguzi unaoshirikisha vyama vingi nchini mwaka 1995. Mbali ya kupoteza majimbo mengi, mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete ameshinda kwa asilimia 61.17  tofauti na mwaka 2005 kilipopata ushindi wa asilimia 80.

Kwa upande wa Vyama vya upinzani vinaonekana kupata mafanikio makubwa kulingana na chama tawala ambacho kimepoteza majimbo kadhaa na kujipunguzia ushindi kilioutarajia.
Mwaka 2005 CCM ambayo ilikuwa ikishikilia majimbo 205 kati ya 239 yaliyopo. Lakini sasa imepoteza majimbo 53 mengi yakiwa kwenye Halmashauri za mikoa na majiji bara na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment